Saturday, August 31, 2013

BONDIA FRANCIS CHEKA ACHUKUA UBINGWA WA DUNIA KWA KUMPIGA BONDIA TOKA MAREKANI KWA POINTI JANA USIKU



Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.

Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.


Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang’anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.

Chukua hiyoooooo…

Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.

Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.

Mpambano ukiendelea.

Wednesday, August 28, 2013

breaking news kwa haters wote wasiyoitakia mema man united

Wayne Rooney set to be offered new Man United deal after rejecting Chelsea [Mail & Telegraph]

Wayne Rooney may have been forced to stay at Manchester United this summer, despite apparently wishing to join up with Jose Mourinho at Chelsea, but the England striker can console himself with a new deal at Old Trafford.

Both the Daily Mail and Daily Telegraph run back page leads on Wednesday confirming that Rooney will sit down to renegotiate his Manchester United contract in the autumn.

After bagging two assists at Swansea in a substitute appearance and with a committed display against Chelsea earlier this week, Rooney is understood to have shown plenty of desire under new Manchester United boss David Moyes.

Despite the urgings of Jose Mourinho, Rooney will not be handing in a transfer request, according to various sources, and looks set for a lengthy stay at Old Trafford.

United hope to sit down with Rooney in three months, provided all is well on the pitch. And chief executive Edward Woodward is also keen to meet with Nemanja Vidic and Nani to discuss new deals around this time.

There are however no guarantees that Rooney will agree to a new deal at Manchester United.

Ian Ladyman writes in the Daily Mail: “Certainly United will not offer Rooney the same £250,000-a-week salary he has earned for the last three years. Any offer will be incentivised and will depend heavily on performances and appearances. Rooney may, therefore, decided to sit it out on his current deal and try to get himself a move somewhere next summer. A move to Chelsea may not be an option in a year’s time, however, as Mourinho will have bought an alternative by then.”

mchezaji wa arsenal angia mkataba na kampuni ya puma ambaye ni santi cazorla

offer offer lipia nusu bei kwa kutangaza na prime advertising magazine upata mafanikio


DRC yaifunga goli moja Cameroon katika mechi ya CHAN


 27 Agosti, 2013 

Timu ya taifa ya Cameroon
Matumaini ya Cameroon ya kufuzu kwa fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani CHAN, itakayoandaliwa nchini Afrika Kusini, imedidimia baada ya kulazwa bao moja kwa bila na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Bao hilo la pekee la na ushindi lilitiwa kimyani kunako dakika ya sabini na Mubele Ndombe ambaye anaichezea klabu ya Vitalo.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo ilishinda kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009, ilitawala mechi hiyo na kwa sasa wanapigiwa upato kufuzu kwa fainali hiyo.
Cameroon na DRC zilishindwa katika mechi zao za kufuzu za mashindano yaliyopita katika kanda ya kati, huku Cameroon ikishindwa na Gabon nayo Congo ililemewa na majirani wao Congo-Brazzaville.
Mechi hiyo ilihairishwa kutoka siku ya Jumapili na kucheza Jumatatu usiku baada ya refa wa mechi hiyo, raia wa Sudan kukosa kufika kwa wakati.
Mechi ya raundi ya pili itachezwa mjini Lubumbashi mwishoni mwa juma hili ili kumua timu itakayofuzu kwa hatua ijayo ya fainali hizo za CHAN.

Gareth Bal;e agoma Kufanya mazoezi

28 Agosti, 2013 Gareth Bal;e agoma Kufanya mazoezi 

Gareth Bale
Klabu ya Tottenham huenda ikalazimika kumpiga faini nyota wake anayesakwa na Real Madrid, Gareth Bale baada ya kukosa kufika uwanja wa mazoezi kwa siku ya pili mfululizo.
Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema Bale ni sharti kutimiza wajibu wake licha ya kuwa huenda akajiunga na Real Madrid.
Mabingwa hao wa Uhispania wametangaza azma yao ya kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni themanini na sita, kiasi ambacho ndicho kubwa zaidi duniani kwa klabu yoyote kumnunua mchezaji mmoja.
Bale, mweye umri wa miaka ishirini na minne, alitarajiwa kurejea kambini siku ya Jumanne baada ya timu hiyo kwenda likizoni katika eneo la Marbella.
''Kwa sasa Real inataka kumsajili Bale, ikiwa hilo litatokea tunamtakia kila la heri, lakini kwa kuwa hajafika kambini, hilo ni kosa na sharti airekebishe'' Alisema Villas-Boas.
Bale amehusishwa na klabu ya Real na kocha huyo wa Tottenham anasema usajili huo huenda ukakamilika hivi karibuni.
Klabu ya Tottenham haitaki kumuuza mchezaji huyo hadi pale watakapomsajili atakayechukua nafasi yake.
Ripoti zinasema Tottenham huenda ikamsajili mshambulizi wa klabu ya Roma kutoka Argentina Erik Lamela kuchukua mahala pa Bale.
Bale hajaichezea klabu ya Tottenham au timu ya taifa ya Wales msimu huu kutokana na Jeraha, lakini mapema siku ya Jumatano alitajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Wales itakayocheza mechi ya kufuzu ya kombe la dunia dhidi ya Macedonia na Serbia baadaye mwezi huu.

Wednesday, August 21, 2013

TOTTENHAM KUTUMIA £100 MILLION KWENYE USAJILI - BAADA YA SOLDADO, PAULINHO NA CHADLI - SASA WAJIANDAA KUTUMIA £60M KWA WILLIAN NA LAMELA


Thumbs up: This EXCLUSIVE picture shows Willian arriving at the InerContinental London Park Lane Hotel ahead of his Tottenham medical on Tuesday afternoon. He is set to move to Spurs in a £30m dealThumbs up: This EXCLUSIVE picture shows Willian arriving at the InerContinental London Park Lane Hotel ahead of his Tottenham medical on Tuesday afternoon

Tottenham wanakaribia kutimiza kiasi cha £100million na kupitiliza kwa kutumia kiasi cha £60m kwa ajili ya kuwasaini viungo washambuliaji Willian na Erik Lamela. Wakiwa tayari wameshatumia kaisi cha jumla £57.6m kuwasajili Roberto Soldado, Nacer Chadli, Etienne Capoue na Paulinho, inawezekana sasa usajili wa wawili hawa unaweza ukafungua milango ya kuondoka kwa Gareth Bale. 
Kiungo wa kibrazil Willian tayari amewasili jijini London kwa ajili ya vipimo leo hii - kama picha zinavyoonesha hapo juu, na kiungo huyo mwenye miaka 25 anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake uanzia kesho - kwa dili linaloaminika kufikia £30m.

Winga wa kiargetina Lamela nae anatajwa kuwa na thamani sawa na Willian na baba yake Jose pamoja na wakala wake Pablo Sebbag wamekuwa na mkutano na wakurugenzi wa ufundi wa Spurs - Franco Baldini na wa Roma Walter Sabatini.

HIVI NDIVYO MANCHESTER CITY WALIVYOANZA LIGI KWA KUIZABUA NEWCASTLE MABO 4-0

Friday, August 16, 2013

Mourinho aiwazia mechi ya kwanza

 16 Agosti, 2013

Jose Mourinho kocha wa Chelsea

Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho amesema itakua vigumu kujizuia wakati atakapokaa rasmi katika benchi ya Stamford Bridge kwa pambano lao la kwanza la Ligi Kuu ya Premier dhidi ya Hull City.

Mourinho aliyejunga tena na klabu hiyo kwa awamu ya pili mnamo mwezi wa Juni baada ya kuondoka mwaka September 2007.
"Nitakapoingia katika uwanja wangu,kukaa katika benchi langu pamoja na watu wangu ,itabidi niwe mtulivu kidogo,"Alisema Mourinho,mwenye umri wa miaka 50.
"Itanichukua dakika mbili tatu kutafakari na kabla ya kushughulikia pambano lenyewe ."
Mourinho aliwasili mara ya kwanza Stamford Bridge mwaka 2004, wiki chache tu baada ya kuiongoza Porto ya Ureno kunyakua kombe la mabingwa wa Ulaya.
Alishinda kombe kombe la FA na pia Kombe la ligi mara mbili pamoja na ubingwa wa ligi ya England mara mbili.
Ingawa hakuweza kunyakua kombe la klabu bingwa ya Ulaya akiwa na Chelsea.
Uhusiano wake na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ulizoroteka na akaondoka licha kwamba alibakiza miaka mitatu katika mkataba wake.
Alishinda kombe lake la pili la klabu bingwa ya Ulaya akiwa na Inter Milan ya Italia mnamo mwaka 2010, lakini akaondoka mwaka mmoja baadae kujiunga na Real Madrid ya Uhispania.
Chini ya uongozi wake Real ilimaliza nafasi ya pili katika La Liga katika msimu wake wa kwanza lakini wakashinda ubingwa mwaka mmoja baadae.

Maelfu wajitokeza kuandamana tena Misri 16 Agosti, 2013




Waandamanaji Misri
Maelfu ya wafuasi wa Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wameanza maandamano mengine mjini Cairo, huku kukiwa na hofu ya kuzuka makabiliano zaidi. Maafisa wa usalama wamezingira barabara kuelekea medani ya Ramses ambapo maandamano hayo yalipangwa kufanyika. Maandamano ya sasa yanajiri siku mbili baada ya jeshi kuvunja kambi ambapo wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood walikua wamesalia kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Makabiliano yalizuka na zaidi ya watu 600 wakauawa, maelfu walijeruhiwa.Maandamano zaidi yanaendelea nje ya mji mkuu Cairo na taarifa zinasema watu wanne wameuawa kwenye makabiliano eneo la Ismailia. Polisi wa Misri wameamrishwa kutumia risasi za moto kulijinda na kulinda majengo ya serikali dhidi ya kushambuliwa.

Huku utawala wa mpito ukitangaza hali ya hatari, mwandishi wa BBC aliyeko Cairo amesema taharuki imetanda mji mzima.Maelfu walikusanyika nje ya msikiti mmoja baada ya Muslim Brotherhood kuwaomba wafuasi wao kuandamana baada ya sala ya ijumaa wakiitaja kama siku ya hasira.
Magari ya kijeshi yanashika doria mjini Cairo, na njia ya kuingia medani ya Tahir kitovu cha maandamano ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Hosni Mubarak imefungwa. Huku haya yakiarifiwa wapinzani wa Mohammed Mosri pia wamepanga kuandamana dhidi ya mahasimu wao. Wakati huo huo watu wameombwa kulinda makaazi yao, makanisa na biashara. Wakristo nchini Misri wamekuwa wakilengwa katika siku za karibuni na makundi ya kiisilamu yenye misimamo mikali. Jumla ya makanisa 25, makaazi na biashara yalishambuliwa hapo Jumatano na

Thursday, August 15, 2013

Diddy amkejeli Kendrick Lamar


Mashambulizi dhidi ya Kendrick Lamar yazidi kuongezeka, hasa pale Diddy alipomuwashia moto kupitia Instagram, nakuthubutu kumuingiza Jay Z kwenye mashambulizi hayo.
Lamar amejikuta katika mashambulizi kutoka kwa Rappers mbali mbali ndani ya masaa 34 baada ya kuvuja kwa ngoma ya Big Sean "Control" ambapo ndani yake kuna mistari yake iliyokuwa ikiwaponda ma-rapper hao na kudai kuwa yeye ni King wa New York.
Diddy ameamua kumshambulia kwa kutumia picha yake akiwa na Jay Z (Mabosi wengine wa NY) wakicheka huku akiambatanisha na maneno yanayomkejeli Kendrick Lamar
"Nakisha Kendrick akasema "mimi ni King wa NewYork"
Diddy sio wa kwanza kumrudishia mashambuliz Lamar, NBA Legend mwenye miaka 67 Phil Jackson aliachia maneno kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya Lamar kumtaja kwenye mashairi hayo

Kendrik Lamar ageuka Ney wa mitego, awageuza mbogo wanahiphop kibao baada ya kudondosha nuclear bomu kwenye "control"


0813_kendrick-lamar_getty2


Kendrick Lamar azua gumzo kupitia mitandao mbali mbali (on fire) baada ya kudondosha verse ya moto hatari na isiyo na huruma ndani ya ngoma aliyoshirikishwa na Big Sean "Control" na kutokuwaacha Drake, J Cole, Asap Rocky, Wale, Pusha T, na Meek Mill, Big K.R.I.T, mbali na hasira zake pale alipowachana ndani ya verse hiyo na kujitamba kuwa yeye ndio king wa NY pamoja na king wa cost.

"I'm usually homeboys with the same niggas I'm rhymin' with," 
 "But this is Hip Hop and them niggas should know what time it is. That goes for Jermaine Cole, Big K.R.I.T, Wale, Pusha T, Meek Mill, ASAP Rocky, Drake. I got love for you all but I'm tryin' to murder you niggas. Trying to make sure your core fans never heard of you niggas [and that] they don't want to hear not one more noun or verb from you niggas. What is competition? I'm trying to raise the bar high." 

Mistari hiyo imefata baada ya Lamar kudai kuwa Rappers wapya sasa hivi wameachwa nje ya mijadala kibao ambayo ameisikia

"I heard the barbershops be in great debates all the time," Lamar amesema kwenye ngoma hiyo. "About who's the best emcee? Kendrick, Jigga and Nas, Eminem, Andre 3000. The rest of y'all new niggas [are] just new niggas. Don't get involved." 

Ngoma hiyo "Control" ime-leak siku ya jumatatu na inasemekana kutokuwepo kwenye album ya Big Sean 

isikilize hapa...onyo.. its dirty

Hatimaye Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) arejea kazini, anazindua movie yake ya kwanza tangu kutoka jela tarehe 30 August

Muigizaji Elizabeth Michael (LULU) anatarajia kuachia movie yake ya kwanza tangu alipotoka jela "Foolsh Age" siku ya tarehe 30 mwezi wa nane katika ukumbi wa Mlimani City huku kukiwa na wasanii wa muzini pamoja na Jay Dee na Machozi Band ambao watasindikiza uzinduzi huo.

hotlulumichaelNina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukimbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS

Wednesday, August 14, 2013

Walter Chilambo kwa Ney Wamitego: Siwezi kutangaza mali zangu ila niko fiti na ninaishi ninavyotaka mimi kwa ushauri na baraka za wazazi wangu



Mshindi wa Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo amefunguka jinsi alivyojiskia baada ya kuiskia ngoma ya Rapper Ney wa Mitego "Salam Zao" pamoja na interview aliyoifanya kwenye kipindi cha XXL , jumatano ya wiki iliyopita.
Walter leo hii kupitoa kipindi hicho hicho cha XXL amesema kwake yeye ni Faraja, kwasababu yeye ni msanii mpya na kutajwa na msanii mkubwa kama Nay ni vizuri maana hujui amekiona nini kwake zaisi inatengeneza attention kwake yeye Chilambo.


Kuhusu milioni 50, ambazo Ney anadai haoni zinapopita maana wasanii wote wa BSS wamepigika tu, Walter amesema, amepewa zote bila utata, na kuhusu Kutokumiliki vitu vya thamani, akasema kwamba hawezi kutangaza ana miliki mali gani, ila yuko fiti kiuchumi na anaishi anavyotaka yeye kwa ushauri wa wazazi na baraka za mungu.




 Ndani ya ngoma hiyo Nay alidai muandaaji wa shindano la Bss Madam Rita hajatoa kitita cha shilingi milioni 50 zilizo tangazwa kutolewa kwa mshindi washindano hilo.

"Hizi salam ziende kwa Madam Rita na Bongo Star search,
mshindi analipwa nini mbona kama maguashi,
namwona Walter Chilambo kapigika kama Zamani,
Haji Ramadhani kachoka yuko Kitaani,
milioni Hamsini zao anazila Nani?
Acheni ubabaishaji wekeni mambo Hadharani,

Ney hakuishia hapo, kwenye Outro Nay Wa Mitego anamaliza kwa kusema Walter Chilambo Niaje Mwanangu, Najua Una hali mbaya Kiuchumi, milioni hamsini Huna Hata Baiskeli? Huna wewe hizo mfikishie salam Madam Rita mwambie sina tatizo nae, 





ukatili aliyofanyiwa owner wahomeshoping center: Mmiliki wa Home Shopping Center akiwa South Africa kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali


MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko  Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hali yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili liko salama.
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.

Baada ya mashabiki kurusha makopo stejini kisa Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zinazosemekana za kushelewa kwake kupanda


Baada ya umati wa watu waliohudhuria show ya Platnum wakirusha makopo stejini baada ya Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zilitajwa kupelekea kuchelewa kwake.
mtandao wa kenya Ghafla umeripoti kuwa Diamond alichelewa kwasababu alikua akijifanya "Diva" pale ambapo kwa maksudi alijichelewesha Tanzania na hivyo kuchelewa ndege kuelekea Kenya.
Baada ya kuchelewa ndege Diamond alidai aletewe ndege binafsi (Private Jet) na National Media Group (NMG) ambapo iliwabidi wafanye hivyo.
So you wonder what led to Diamond being delayed?Apparently the concert was delayed because the 'Nataka Kulewa' singer was being a total diva.It is said that Diamond deliberately stalled in Tanzania  therefore missing his plane to Kenya, he then demanded a private jet from the Nation Media Group. NMG had to bend over backwards  and charter a  private jet for the Tanzanian Superstar.
Mda mfupi baada ya Diamond kutua Mombasa aligoma ku-check in katika hoteli aliyoandaliwa (Mombasa Beach Hotel)  ambapo ndipo show ilipokuwa ikifanyika na kusisitiza kuchukuliwa presidential  suite White Sands Hotel ambayo iliwagharim mkwanja mrefu NMG.
Baada ya mahitaji yake kukamilishwa ndio Diamond alikubali kupanda stage, ila baada ya kukitifua mbaya stejini  kama wa kweli kwa show na perfomance ya hatari na kuwaacha watu wakiwa na historia isiyofutika leo wala kesho, show ambayoinayoweza kuelezeka kama ya ki legendary.Mashabiki walitulia na kuimba nyimbo zake mwanzo mwisho..
mtangazaji katika video hii badala ya kusema Nasibu Abdul yeye kasema Kassim lol

Rooney haendi kokote asema Moyes



Wayne Rooney
Kocha mpya wa Manchester United David Moyes, amekariri kuwa nyota wake Wayne Rooney atasalia na klabu hiyo na kamwe hana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anarejea nyumbani kutoka Thailand ambako timu hiyo imepiga kambi kambla ya kuanza kwa msimu, kutokana na jeraha la mguu.
Kumekuwa na fununu kuwa mchezaji huyo huenda akakihama klabu hiyo, licha ya Moyes kusisitiza kuwa Rooney hauzwi kwa lolote lile.
Klabu ya Chelsea, vile vile wako nchini Thailand na kocha wao mpya Jose Mourinho aliulizwa ikiwa ana nia ya kumsajili Rooney.
Lakini Mourinho alisema kwamba hana mazoea ya kuzungumza kuhusu wachezaji wa klabu nyingine lakini amekiri kuwa anampenda Rooney.
Kwa upande wake Moyes alisema kocha huyo wa Chelsea ana nia ya kumsajili mchezaji huyo ila hataki kusema wazi wazi.
Rooney, ambaye ameifunguia Manchester United magoli 197, baada ya kucheza mechi mia nne na mbili anatarajiwa kusalia nje ya uwanja wa muda wa wiki mbili zijazo kutokana na jeraha hilo na wala sio mwezi mmoja

Kenya yapata dhahabu ya kwanza Moscow 1


Edna Kiplagat akimaliza mbio mjini Moscow
Mashindano ya mbio za dunia yameanza hii leo mjini Moscow Urusi.
Bingwa mtetezi wa mbio za marathoni kwa upande wa wanawake Edna Kiplagat kutoka Kenya ametetea taji lake mapema jumamosi asubuhi baada ya kushinda medali ya dhahabu.
Kiplagat ameshinda mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 25 na sekunde 44.
Valeria Straneo wa Italia ameshika nafasi ya pili licha ya kuongoza kwa muda mrefu kwenye mbio hizo, lakini Kiplagat alianza kumuacha walipofika kilometa 40 na kumaliza mbio kwa zaidi ya sekunde 15 nyuma ya Straneo.
Kayoko Fukushi wa Japan ameshika nafasi ya tatu na kuchukua medali ya shaba.
Hii ni medali ya kwanza ya Kenya ya dhahabu kwenye mashindano hayo ya dunia yanayoandaliwa na shirikisho la riadha duniani IAAF.

Kiongozi wa kiisilamu atoweka Zanzibar

asiwasi umetanda kisiwani Zanzibar kufuatia kutoweka kwa kiongozi wa kidini Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Watu wawili wametiwa nguvuni waliohusika na maandamano na ghasia zilizosababisha uharibifu mkubwa kisiwani humo.
Kuna hofu kuwa kiongozi huyo huenda amekamatwa na polisi na anazuiliwa Tanzania bara kutokana na kuwa amepinga utawala wa chama tawala cha Tanzania bara CCM.
Kwingineko, hapo jana polisi nchini Tanzania walimkamata mhubiri mwenye utata anayetuhumiwa kwa kuchochea vurugu wiki jana , na kusababisha maandamano mapya.
Kulingana mkuu wa polisi, Suleiman Kova ,Sheikh Ponda Issa Ponda, mkuu wa Jumuiya ya waislamu, vuguvugu ambalo halitambuliki na serikali ya Tanzania, alikamatwa kwa kuchochea vurugu.
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda, mini Dar es Salaam, inakuja baada ya kukamatwa kwa watu 31 waliozua vurugu na kupora mali ya watu wakati waandamanaji walijawa na ghadhabu na kuandamana wiki jana wakiharibu makanisa kadhaa mjini humo.
Maandamano ya wiki jana yalisababishwa na tetesi kuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliikojolea Quran.
Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake kufanya maandamano kinyume na sheria na kutoa wito wa ghasia na umwagikaji damu mjini Dar es Salaam na nchini kote.

Taarifa zinazohusiana

BAKWATA laitisha uchunguzi kuhusu Ponda



Sheikh Ponda
Baraza la waisilamu Tanzania limeunga mkono kauli ya Jumuiya ya taasisi za kisilamu za kuitaka serikali kuchunguza kwa kina tukio lililopelekea kupigwa risasasi kwa mhubiri wa kiisilamu Sheikh Issa Ponda. Taarifa imetolewa na kaimu mufti wa Tanzania Al Had Musa Salum.
Pamoja ya kwamba (BAKWATA) limekuwa likipingana na misimamo ya Sheikh Ponda limesema serikali ilikuwa na nafasi ya kumkamata Ponda kwa kufuata mkondo wa sheria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam, Baruan Muhuza, sheikh huyo ambaye amekuwa katika mivutano ya mara kwa mara na serikali ya nchi hiyo alipigwa risasi baada ya kutokea vurugu kwenye mkutano wa mawaidha ya baraza la sikukuu ya Idd el Fitr.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhajj Mussa Kundecha, amewaambia waandishi wa habari mjini humo kuwa endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya Tanzania.
Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam akiuguza jeraha la risasi huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.
Msemaji wa Jeshi la polisi nchini humo Advera Senso ameiambia BBC mjini Dar es Salaam kuwa jeshi lake kwa kushirikiana na jukwaa la haki jinai wameunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akikana kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi na polisi.
Senso amewalaumu wafuasi wa Sheikh Ponda kwa kuwazuia askari kumkamata Sheikh huyo kwa kuwarushia mawe; hatua iliyosababisha askari hao kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya na hata hivyo wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha kiongozi huyo wa kidini.
Taarifa za jumuiya hiyo ambayo inajulikana zaidi Tanzania kama Shura ya Maimamu zinasema kuwa Sheikh Ponda ambaye polisi wanasema walikuwa wakimtafuta kwa tuhuma za kutoa matamko ya uchochezi, alisafirishwa usiku kutoka mji wa Morogoro hadi Dar es Salaam zaidi ya kilomita 200.
Sheikh Ponda kwa sasa anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja alichohukumiwa mapema mwaka huu baada ya kukutwa na makosa kadhaa ikiwemo uchochezi wa kuharibu mali za watu.

44 wauawa kinyama msikitini, Nigeria



Maiduguri ni moja ya majimbo yaliyowekewa sheria ya hali ya hatari
Takriban waumini 44 wameuawa kwa kupigwa risasi wakiwa msikitini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa maafisa wa jimbo la Borno.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maombi ya asubuhi Jumapili , ingawa taarifa zimejitokeza Jumatatu , kutokana na hitilafu ya mawasiliano kwani jimbo hilo liko chini ya sheria ya hali ya hatari.
Shambulizi lilifanyika katika mji wa Konduga, ulio umbali wa kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo , Maiduguri.
Washambulizi wanasemekana kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji la Boko Haram, ambalo liliwaua maelfu ya watu tangu mwaka 2009.
Gazeti la Daily Post, liliripoti kuwa watu wengine 26 walikuwa wanatibiwa kwa majeraha waliyopata wakati wa shambulizi hilo hospitalini Maiduguri.
Mwanachama wa kikundi cha vijana kinachotoa ulinzi kwa raia, aliambia shirika la habari la Associated Press, kuwa wapiganaji wao wannne waliuawa walipojaribu kutoa kilio cha kutaka usaidizi.
Raia wengine kumi na wawili, waliuawa katika kijiji cha Ngom kinachopakana na Maiduguri.
Rais Goodluck Jonathan alitangaza sheria ya hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskazini Mashariki mwa nchi mnamo mwezi Mei wakati wanajeshi walipofanya operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Boko Haram linapigania eneo la Kaskazini mwa nchi likitaka kujitawala kwa kutumia sheria za kiisilamu.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos, anasema kuwa wakati kundi hilo limekuwa likishambulia makanisa, pia limekuwa likishambulia misikiti.
Habari za mashambulizi hayo zilijitokeza wakati kanda ya video ya kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, ilipotolewa akidai kundi hilo kuhusika na mashambulizi hayo ikiwemo kushambulizi dhidi ya vituo vya polisi na kambi za jeshi.

Wafuasi wa Morsi watawanywa Misri





Waandamanaji wanaomuunga mkono Morsi
Polisi nchini Misri, wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi wakati wa maandamano yao mjini Cairo.
Vikosi vya usalama viliingilia maandamano hayo baada ya wafuasi wa Morsi kukabiliana na mahasimu wao wa kisiasa.
Walioshuhudia vurugu hizo walirushiana mawe na chupa huku watoto na wanawake wakikimbilia usalama wao.
Morsi aliondolewa mamlakani na viongozi wa jeshi mwezi Julai kufuatia maandamano makubwa sana.
Tangu hapo jeshi limeweka serikali ya mpito.
Wafuasi wa Morsi aliyeingia mamlakani baada ya vuguvugu la kiisilamu la Brotherhood kushinda uchaguzi wa rais, wanakataa kukubali serikali mpya ya mpito wakisisitiza kuwa lazima rais wao arejeshwe mamlakani.
Vurugu za Jumanne zilianza wakati wafuasi wa Morsi, walipotembea hadi sehemu moja ya Cairo ambako watu wengi wanapinga vuguvugu la Muslim Brotherhood.
Waandamanaji hao walijaribu kuingia katika ofisi za wizara moja ingawa polisi waliwalazimisha kuondoka kwa nguvu.
Wakaazi wa eneo hilo walianza kuwakejeli waandamanaji na hapo ndipo polisi walipoingilia mzozo huo.
Mamilioni ya wamisri waliandamana kumtaka Morsi aondolewe mamlakani ingawa wadadisi wanasema kuwa kuondolewa kwake kunaonekana kuzorotesha migawanyiko ya kisiasa iliyoko kwa sasa.
Wafuasi wake wamekuwa wakipiga kambi mjini Cairo wakitaka arejeshwe mamlakani.
Maafisa wa usalama walitishia kuondoa mahema waliyoweka wafuasi wa Morsi ambako wamekuwa wakipiga kambi lakini wakabatili uamuzi wao baada ya kuamua kuuakhirisha.

Monday, August 12, 2013

Gervinho akamilisha usajili AS Roma




Gervinho akishangilia moja ya mabao yake Arsenal

Usajili wa wachezaji mbalimbali unazidi kushika kasi barani ulaya.

Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast,Gervais Lombe Yao Kouassi maarufu kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As Roma ya Italia.
Uhamisho huo wa Gervinho umetajwa kuwa wa pound milioni 8 walizopewa Arsenal.
Gervinho alihamia Arsenal mwaka 2011 akitokea Lile ya Ufaransa.
Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.
Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia Seria A utakuwa changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Taarifa zinazohusiana

Wednesday, August 7, 2013

Moto mkubwa wateketeza uwanja wa JKIA



Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ukiteketea
Safari za ndege za ndani ya nchi nchini Kenya zinatarajiwa kurejea kama kawaida baadaye leo baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya uwanja rasmi wa kimataifa wa ndege nchini humo JKIA.
Msemaji wa ikulu ya rais, Manoah Esipisu alisema kuwa ndege za mizigo zitaanza kusafiri lakini akaongeza kuwa serikali haiwezi kusema bayana ni lini safari za kimataifa za ndege zitarejea kama kwaida.
"Tunatarajia kuwa safari za ndege ndani ya nchi zitaweza kurejea kama kawaida baadaye leo, '' alisema Esipisu.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta awali leo ulikua umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Moto huo hata hivyo ulidhibitiwa
Hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.
Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia ziliahirishwa wakati zengine zikielekezwa kwenda Mjini Mombasa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Huu ni moto mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta wenye kutumiwa na wasafiri wengi zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati .
Taarifa za awali zilionyesha kuwa moto huo ulianzia kwenye eneo la uhamiaji katika kitengo cha kupokea wageni kabla ya kusambaa hadi maeneo ya ushuru na mizigo ya abiria.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana , lakini maafisa wa ngazi ya juu wa serikali wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta walitembelea uwanja huo na kutoa wito uchunguzi ufanyike mara moja. Hata hivyo hawakutoa ishara yoyote ni lini uwanja huo utafunguliwa tena .
Shirika la ndege la kenya -Kenya Airways, ambalo ni kubwa zaidi katika kanda ya Afrika limefuta safari zake zote na kuelekeza ndege zinazoingia nchini katika mji wa Mombasa . Tayari hisa za ndege zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 2 . Ndege za kimataifa ambazo zilitakiwa kuondoka leo asubuhi ziliruhusiwa kuondoka bila wasafiri.

Diamond Platnumz akishoot video South Africa






Mahakama yamuamuru 50 Cent kusalimisha bunduki zake zote


50 Cent ambae jana amekutwa hana hatia kwa mashtaka ya unyanyasaji wa nyumbani  (domestic violence) baada ya kudaiwa kumshambulia mama wa mtoto wake nyumbani kwake (Juni),  licha ya kuonekana hana hatia lakini bado hakimu alimuamuru 50 Cent kukaa mbali na mama huyo  na kusalimisha bunduki zake zote.

Kutokana na protective order, 50 pia amepigwa marufuku kuwasiliana na model Dafne Joy - anaedaiwa kuwa ni mama wa mtoto wake wa pili, kwa njia yoyote, na lazima akae nae mbali kwa angalau yadi 100 wakati wote.
   Fiddy alishtakiwa kwa unyanyasaji wa majumbani baada ya kudaiwa kumpa mateke Joy na kisha kuharibu  rundo la mali,  LA.

Wakati wa ghasia, inasemekana Fiddy (38) uvunja chandeliers, samani, TV na taa.
Joy aliwaambia wachunguzi kuwa 50 ni baba wa mtoto wake - ingawa 50 hajawahi kukiri hadharani kuwa kazaa mtoto na Joy.






Fabregas asema hataki kurejea England


 16 Julai, 2013 - Saa 17:23
Cesc Fabregas
Mcheza kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amesema hana nia yoyote ya kuihama klabu hiyo na kurejea tena nchini England.
Hayo ni kwa mujibu wa kocha wake Tito Vilanova.
Klabu ya Manchester United siku ya Jumatatu iliwasilisha ombi la kutaka kumasajili nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini Vilanova amesema mchezaji huyo anataka kusalia nchini Uhispania kwa sasa.
''Ni ishara nzuri kwa klabu yoyote kupata maombi kutoka kwa vilabu vingine, vinavyotaka kuwasajili wachezaji wake, lakini Fabregas amesema anataka kusalia'' Alisema kocha huyo.
Vilanova ameongeza kusema kuwa'' Fabregas hataki kujiunga na timu zingine kwa sababu ya pesa au kutokana na muda wake wa kucheza uliosalia. Anafahamu huku kuna ushindani mkali, lakini ni uamuzi wake kusalia na Barcelona. Kwa sasa nimetulia''.
Kufikia sasa Barcelona halijasema lolote rasmi kuhusiana na ombi hilo la Manchester United, ambalo linaaminika kuwa chini ya dhamana kamili ya mchezaji huyo.
Fabregas alikuwa mchezaji mchanga zaidi wa Arsenal wakakti aliocheza dhidi ya Rotherham United wakati wa mechi ya kombe la ligi mwaka wa 2003 akiwa na miaka kumi na saba na siku mia moja na sabini na saba.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Arsenal walioishinda timu ya Manchester United kupitia mikwaju ya penalti kwa fainali ya kombe la FA mwaka wa 2005.
Vile vile Fabregas, anaichezea timu ya taifa ya Uhispania na aliisaidia kunyakua kombe la dunia na pia kuwa mabingwa wa bara Ulaya mara mbili.
Alijiunga na Arsenal mwaka wa 2003 akiwa na umri wa miaka kumi na sita.
Fabregas aliichezea Arsenal mechi 303 na kufunga magoli 57, kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 25.4 kwa mkataba wa miaka mitano kwa wa 2011

man united itafanikiwa kumsajili fabregas?


Man United itafanikiwa kumsajili Fabregas?

 23 Julai, 2013 
Cess Fabregas
Klabu ya Barcelona imeiambia Manchester United kuwa haina nia ya kumuuza nyota wake Cesc Fabregas.
Manchester United, imethibitisha kuwa iliwasilisha tena ombi la kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni thelathini, lakini ripoti zinasema kuwa ombi hilo limekataliwa.
Rais wa Barcelona Sandro Rossel, amekariri kuwa klabu hiyo haina nia ya kumuuza mchzaji huyo kwa klabu yoyote.
Kocha wa Manchester United, David Moyes amenukuliwa akisema huenda wasifanikiwe kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo Moyes amekiri kuwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward, angali anafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa wamemsajili mchezaji huyo.
Mara ya kwanza United iliwasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Barcelona.
David Moyes Kocha wa Manchester United
Siku mbili tu baada ya United kuwasilisha ombi hilo, Woodward alikatiza ziara yake nchini Australia na kurejea nyumbani kuongoza mikakati ya kumsajili Fabregas, kabla ya muda wa mwisho wa usajili kukamilika.
Barcelona haijatoa taarifa yoyote, lakini kuna habari kuwa huenda matatizo yanayokumba klabu hiyo kwa sasa yamechangia pakubwa uamuzi huo kukataliwa.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Haijulikani ikiwa uamuzi wa Chelsea wa kutaka kumsajili mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney umechangia klabu hiyo kutaka kumsajili Fabregas.

Mipango ya kuleta amani ilioanzishwa na jumuiya za kimataifa zagonga mwamba misri ,kwa habari zaid soma hapa

Juhudi za kimataifa zagonga mwamba Misri

7 august 2013
Wajumbe wa kimataifa wakifanya mazungumzo na rais wa mpito Adly Mansour
Rais wa mpito nchini Misri, anasema kuwa juhudi za kimataifa kutuliza mgogoro wa kisiasa nchini humo ambao ulitokana na kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi, zimegongwa mwamba.
Adly Mansour na washirika wake walioko kwenye jeshi, wamekuwa wakishauriana na wajumbe wa kimataifa kutoka Marekani, Muungano wa Ulaya , Qatar na Milki za kiarabu.
Zaidi ya watu 250 wameuawa kwenye mgogoro huo wa kisiasa tangu Morsi kuondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai baada ya maandamano ya umma.
Maseneta wawili wa Marekani siku ya Jumanne waliitisha mazungumzo kati ya serikali ya mpito na vuguvugu la Muslim Brtherhood
Lakini serikali ya mpito hii leo ilitangaza kuwa mazungumzo ya kidiplomasia yamefika kikomo leo.
Iliongeza kusema kuwa juhudi hizo hazijafanikisha chochote.

Brotherhood walaumiwa

Serikali imesema kuwa inalaumu vuguvugu la Muslim Brotherhood kwa kutofanikiwa kwa juhudi za amani na matukio mengine yanayohusu utovu wa usalama na ukiukwaji wa sheria.
Mjumbe wa Marekani Bernardino Leon na mwenzake naibu waziri wa mambo ya nje wamekuwa Misri kwa siku kadhaa kufanya mazungumzo ya kupatanisha pande hizi mbili katika mgogoro huu.
"tutajaribu kadri ya uwezo wetu kuhakikisha watu wanashauriana,'' alisema msemaji wa EU Michael Mann.
"ni Muhimu kuona kuwa kunakuwa na kipindi cha mpito chenye kuzingatia demokrasia...tutaendelea na juhudi zetu,'' aliongeza msemaji huyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi amekuwa mjumbe wa hivi karibuni aliyetarajiwa kufanya mzungumzo na mwenzake wa Misri, waziri mkuu na rais wa mpito pamoja na maafisa wengine mnamo Jumatano

Je Tsvangirai alijichimbia kaburi lake?

Je Tsvangirai alijichimbia kaburi lake?

 6 Agosti, 2013 - Saa 12:11 GMT

Morgan Tsvangirai analaumiwa na wengi kwa masiabu yanayomkumba
Minong'ono ilikithiri kwa miaka mingi. Wengi wakasema sio mjanja . Anapenda kucheza Golf sana . Ndio ni jasiri kwa uhakika , lakini mtu asiye na mikakati.
Huyu ndiye mwanasiasa aliyejaribu mara tatu kuwa rais wa Zimbabwe lakini hakuwahi kufua dafu hata siuku moja.
Morgan Tsvangirai, sasa anatupia macho hali ya kusahaulika kisiasa kufuatia chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliokamilika wiki jana, na kuna watu wengi wanahisi kuwa alipaswa kushindwa.
Hata ikiwa madai anayoyatoa kuwa kura ziliibwa na chama tawala ZANU-PF yatathibitishwa na majirani wa Zimbabwe wakitaka uchaguzi kurejelewa, rais Robert Mugabe hajaona sababu kubwa ya kuhofia upinzani mkubwa kwa utawala wake.

Sasa kwa nini Tsvangirai alaumiwe?

Wadadisi wanasema kosa kubwa ambalo yeye na chama cha MDC walifanya, ni uamuzi wake wa kujiondoa kutoka kinyang'anyiro cha mwaka 2008 kwa sababu ya ghasia zilizotokea baada ya utata uliofuata uchaguzi huo na kujiunga na rais Mugabe katika serikali ya Muungano.
Na kama wanavyosema , Tsvangirai alimuwezesha mpinzani wake kushikilia wadhifa wakati yeye mwenyewe hakuwa na ushawishi mkubwa.
Hatua ya Tsvangirai ilizua utata mkubwa na kupingwa na washirika wake wa karibu wa MDC - ingawa kunao wanaosema kuwa hatua yake ilikuwa sawa.
Wafuasi wa Mugabe wakisherehekea ushindi wake wiki jana
Zimbabwe ilikuwa katika hali ngumu - uchumi ulikuwa unaporomoka.
Kwa kujiunga na serikali ya Muungano, Tsvangirai alionekana kutojali maslahi ya wafuasi wake wakati yake akiyapa kipaombele.
Hata hivyo kosa kubwa ambalo Tsvangirai alifanya ni kutojitetea wakati akiwa katika serikali ya Muungano na Mugabe.

Uhusiano wa dhuluma

Katika siku ya kwanza ambapo makamanda wa jeshi la Mugabe walipokataa kumpigia saluti kama waziri mkuu wa Zimbabwe, Tsvangirai angeteta na kupinga hilo na kisha kuwaambia wanadiplomasia waliokuja kwenye mkutano huo, walikuwa wanapoteza muda na kisha kujiondoa kwenye mkataba wa kugawana mamlaka.
Lakini kwa kukosa kujiondoa, alimuonyesha Mugabe kuwa angeendelea kuwa katika serikali ambayo haimpi heshima zake na yeye ni mwanachama mwenye ushawishi mdogo katika serikali ya Muungano na kuwa angestahimili dhuluma katika uhusiano wao ambao ulifika mwisho wake wiki jana.
Bwana Tsvangirai badala yake aliendelea kusisitiza umuhimu wa kupatanisha watu akiwa na matumaini kuwa Mugabe angezingatia demokrasia.
Muungano tawala ulionekana kumdhulumu Tsvangirai lakini kwa nini hakujiondoa?
Lakini badala yake, Mugabe -alimzuia , akabadili sheria akiendelea kushikilia mamlaka hadi alipoitisha uchaguzi mkuu kwa maslahi yake mwenyewe .
Baadhi wanasema kuwa Tsvangirai angejiondoa kwenye uchaguzi kabla ya uchaguzi kufanyika wakati ilipokuwa wazi kuwa Mugabe hangetoa muda kwa wapiga kura kujiandaa kwa uchaguzi, mfano kujisajili au hata kufichua daftari la wapiga kura ambalo wengi wanasema lilikuwa na dosari nyingi.
Lakini badala yake Tsvangirai aliitikia wito wa Mugabe wa kufanyika uchaguzi ambao sasa anasema ulijaa makosa na wizi wa kura.
Je ilikuwa hatua nzuri au ilikuwa ishara ya kutojua au kujiamini kupita kiasi?
Wakati mmoja hilo swali litajibiwa na wakereketwa wa chama chake na mwishowe wapiga kura.

LIONEL MESSI,FRANK RIBERY CHRISTIANO RONALDO KUWANIA TUZO YA UEFA

Ni Messi, Ronaldo au Ribery tuzo ya UEFA

 6 Agosti, 2013 


Ronaldo na Messi kwenye tuzo zilizopita

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery watachuana kuwania tuzo ya shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA kuwa mchezaji bora wa Ulaya katika msimu uliopita..

UEFA ilitangaza majina ya wanasoka hao watatu siku ya Jumaanne baada ya awali kutangaza orodha ya wachezaji kumi bora walioteuliwa na waandishi habari wa nchi wanachama za UEFA..
Ribery ni miongoni mwa wachezaji wanne wa klabu bingwa ya Ulaya Bayern Munich wanaotoa changamoto kwa wachezaji wawili mashuhuri wanaosifiwa katika kandanda ya barani Ulaya.
Tuzo hiyo itatolewa Agosti 29 mwaka huu 2012 wakati wa droo ya michuano ya klabu bingwa ya Ulaya mjini Monaco baada ya kupigiwa kura na jopo la wanahabari..
Messi alishinda tuzo ya kwanza misimu miwili iliyopita na mwenzake wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta alishinda mwaka jana.

Moto mkubwa wateketeza uwanja wa JKIA nchini kenya

Moto mkubwa wateketeza uwanja wa JKIA

 7 Agosti, 2013 

Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ukiteketea
Safari za ndege za ndani ya nchi nchini Kenya zinatarajiwa kurejea kama kawaida baadaye leo baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya uwanja rasmi wa kimataifa wa ndege nchini humo JKIA.
Msemaji wa ikulu ya rais, Manoah Esipisu alisema kuwa ndege za mizigo zitaanza kusafiri lakini akaongeza kuwa serikali haiwezi kusema bayana ni lini safari za kimataifa za ndege zitarejea kama kwaida.
"Tunatarajia kuwa safari za ndege ndani ya nchi zitaweza kurejea kama kawaida baadaye leo, '' alisema Esipisu.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta awali leo ulikua umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Moto huo hata hivyo ulidhibitiwa
Hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.
Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia ziliahirishwa wakati zengine zikielekezwa kwenda Mjini Mombasa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Huu ni moto mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta wenye kutumiwa na wasafiri wengi zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati .
Taarifa za awali zilionyesha kuwa moto huo ulianzia kwenye eneo la uhamiaji katika kitengo cha kupokea wageni kabla ya kusambaa hadi maeneo ya ushuru na mizigo ya abiria.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana , lakini maafisa wa ngazi ya juu wa serikali wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta walitembelea uwanja huo na kutoa wito uchunguzi ufanyike mara moja. Hata hivyo hawakutoa ishara yoyote ni lini uwanja huo utafunguliwa tena .
Shirika la ndege la kenya -Kenya Airways, ambalo ni kubwa zaidi katika kanda ya Afrika limefuta safari zake zote na kuelekeza ndege zinazoingia nchini katika mji wa Mombasa . Tayari hisa za ndege zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 2 . Ndege za kimataifa ambazo zilitakiwa kuondoka leo asubuhi ziliruhusiwa kuondoka bila wasafiri.