Sunday, August 31, 2014

FIFA:Platini asema hatampinga Blatter

Michel Platini amewaambia wajumbe wa bara Uropa kuwa hatampinga Blatter katika uchaguzi wa urais wa FIFA mwakani
Rais wa shirikisho la soka barani Uropa Uefa Michel Platini hatompinga Sepp Blatter katika kura za kuwania rais wa FIFA mwakani.
Rais huyo wa UEFA ambaye ni raiya wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 59 alikuwa ameonesha niya ya kumpinga Blatter lakini leo amewaambia wajumbe wa UEFA huko Monte Carlo kuwa anataka kuihudumua UEFA kikamilifu.
Mwanakamati wa Fifa Michel D'Hooghe alisema '' ni jambo la kutoa moyo kwani inamanisha kuwa mwaka huu hatutakuwa na ubishi kati ya UEFA na FIFA''Platini amewambia wajumbe hao 54 kuwa licha ya yeye kutaka kuwe na ''hewa safi katika FIFA'' anapendekeza kujitolea kimasomaso katika uongozi wa UEFA.
Blatter, 78,ameongoza FIFA tangu mwaka wa 1998, lakini amekumbwa na upinzani mkubwa baada ya kuibuka tuhuma za hongo katika uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.

Rais wa Fifa Blatter akizungumza na Michel Platini
Joto la kisiasa katika FIFA lilipanda majuzi baada ya Blatter kutangaza kuwa atawania nafasi ya kuongoza FIFA kwa mhula wa tano.
Kujiondoa kwake sasa kunamwacha Blatter akikabiliana na aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA wa zamani Jerome Champagne.
Wagombea wanapaswa kutangaza niya yao kuanzia Januari 2015 hata hivyo Platini atalazimika kusubiri hadi baada ya miaka mingine minne ilikuwania urais mwaka wa 2019.
Platini, aliiongoza Ufaransa kutwaa taji la Uropa mwaka wa 1984.
Ameiongoza Uefa tangu mwaka wa 2007.
Anatarajiwa kuiongoza Ufaransa kupanga na kuandaa mchuano wa Euro 2016 mbali na makala ya mwaka wa Euro 2020 .

No comments:

Post a Comment