Friday, July 17, 2015

50 CENT AMEFILISIKA...


RAPA 50 Cent ameandikisa kurasa 11 juu ya kufilisika kwake katika Mahakama ya Connecticut leo.
Katika karatasi zilizowasilishwa mahakama ya Wafilisika mjini Hartford, Conn., rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III ameripoti mali zake na madeni ambavyo ni dola za Kimarekani kati ya Milioni 10 na Milioni 50 kwa mujibu wa WTIC.
Wiki iliyopita, Mahakama ya New York ilimtaka Jackson kulipa dola Milioni 5 kwa mwanamke aliyemshitaki kwa mkanda wa ngono.
Jackson anamiliki 50 Poplar Hill Drive mjini Farmington, kwa mujibu wa takwimu za kodi, iliyo umbali wa maili 10 kutoka Hartford. 
Jengo hilo limetiwa mnadani kwa miaka sasa, lakini kwa sasa halina soko. Kwa mujibu wa Zillow, nyumba hiyo ina vyumba 21 vya kulala, mabafu 25, na ukubwa wa mita 48,515

No comments:

Post a Comment