Friday, July 17, 2015

Mtanzania mwingine kwenye headlines za soka Ulaya

 
 
Charles Misheto anaingia katika headline tena ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kitanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania, taarifa hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tu toka aliyekuwa beki wa Simba B Emily Mugeta kujiunga na klabu ya Neckarsulm ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi daraja la tano.
Charles Misheto amejiunga katika klabu ya Rabestein ya Ujerumani inayoshiriki Ligi daraja la nne kwa mkataba wa miaka miwili… Hii sio mara ya kwanza kwa Charles kucheza soka nchini humo, aliwahi kucheza katika klabu ya Melbtiz ya nchini humo.
Hata hivyo Charles amewahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga na inashiriki ligi kuu Tanzania bara.
“Ingawa awali nilikuwa nafanya majaribio na timu nyingine, lakini sasa nimefanikiwa kusajiliwa na timu nyingine ya daraja la nne ambayo ilianza kuniwania”>>>> Charles
“Nilikuja hapa, nikafanya nao mazoezi kwa siku mbili, baada ya hapo wamekubaliana na uwezo wangu tumesaini mkataba”>>> Charles
Hii ni habari njema kwa watanzania wote wapenda soka na maendeleo hivyo anaingia katika orodha ya baadhi ya wachezaji wa kitanzania wanaocheza soka nje ya nchi, baadhi yao kama Abdi Kassim anayecheza Malaysia na Mwinyi Kazimoto anayecheza Qatar .

No comments:

Post a Comment